youtube: https://youtu.be/yKcVY-Rlc58
Anayekula Mwili Wangu Lyrics
- Anayekula mwili wangu, na anywaye damu yangu
Anaishi ndani yangu, ‚ye hatakufa milele- Yesu wangu nakuomba, nishibishe na mwilio
Nayo damu yako ninywe, japo sistahili mimi
- Yesu wangu nakuomba, nishibishe na mwilio
- Ndani yangu Mwokozi yumo kwa mwili na damu yake
Ni rafiki yangu kweli nami sitamwacha kamwe - Alikuja kutuokoa, tuliokuwa dhambini
Kwa kifo chake msalabani, naye katupa uzima - Yesu wangu unibariki, nifundishe njia zako
Nipe moyo wa shukrani, nitembee nawe leo
Please follow and like us:
